THE CORPSE OF ANNA FLITZ

Mwili wa Muigizaji Mrembo na maarufu, Anna Fritz, Ghafla unapatikana katika hotel akiwa amefariki, habari juu ya kifo chake zinasambaa duniani kote. 



Pau ni kijana anayefanya kazi hospitali katika chumba cha kuhifadhia maiti, kazi inayompa fursa ya kutazama miili ya wanawake vijana inayoletwa katika chumba hicho cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo.


Siku moja anashangaa wakati mwili wa Anna Fritz, mwigizaji mzuri na wakuvutia, unawasili ili kuhifadhiwa katika hospital, hiyo. Pau baada ya kuupokea mwili wa Anna anavutiwa na mwili huo na kuamua kuupiga picha na kumtumia rafiki yake mmoja, Ivan, ambaye kwa haraka baada ya kuona picha hiyo anafika hospitalini hapo akiwa na Javi, rafiki yake mwingine. 



Wote watatu wakiwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti wakiutazama mwili wa Anna, Ivan anatafakari kuuliza kama inawezekana kubaka maiti na Pau anajibu kuwa lazima mate yatumike kama kilainishi. Alipoulizwa kama anajua hili kutokana na uzoefu wa zamani, Pau anakiri kuwa alibaka maiti ya msichana wa miaka 17 au 18 Hivi karibuni. 

Ivan anaamua kuwa anataka kubaka maiti ya Anna na kuanza kuibaka, na kumfanya Pau kupendekeza atafuata yeye baada ya  ivan kumaliza. Javi anachukizwa na kitendo kile cha kubaka maiti na wanapopendekeza achukue zamu baada ya Pau anakataa.

Wakati wa tendo hilo linaendelea, ghafla Anna anarudi hai na kufungua macho yake wakati Pau anambaka. Anna hawezi kusonga, lakini macho yake yamefunguka. Kwa hofu Pau anapiga mayowe anapotambua hili na wengine kuingia chumbani. Wanaume hao basi wanakabiliwa na chaguzi mbili: Wanaweza kuripoti kufufuka kwa Anna na kukabiliana na mashtaka ya ubakaji, kwa kuwa hakuna njia ambayo Anna angekubali kufanya ngono, au wanaweza kumuua na kuficha uhalifu wao. Wakati Pau na Ivan wote wanataka kuficha uhalifu wao, Javi anawasukuma kumwokoa Anna na kuwataka wawajibike kwa kile walichokifanya. 

Wanaume hao watatu wanabishana na Ivan bila kukusudia anamuua Javi. Baada ya kufa Javi hivyo hakuna wa kuwazuia tena, na Ivan yuko tayari kumuua Anna. Ivan anamshawishi Pau kwamba hakuna njia ambayo Anna angekaa kimya ikiwa ataachwa hai. 

Wanaamua kumziba Anna na shuka ili afe hivyo isibaki alama kwenye mwili wake na Pau ndo anaefanya hicho kitendo. 

Wakati Ivan akiondoa ushahidi kwenye eneo hilo, Pau anasafisha mwili wa Anna na kumfunika shuka jeupe. Akiwa anakaribia kuondoka, Pau anamwambia Anna ajifanye amekufa na inabainika kuwa alighushi mauaji hayo hakumuuwa Anna. 

Ivan anarudi na wote wawili wanatoka chumbani. Wanapokaribia kupanda kwenye lifti, Ivan anaangalia pochi yake na kugundua kuwa alisahau kadi yake kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Pau bila mafanikio anajaribu kumshawishi aondoke badala ya kuirudia kadi yake, akisema ataichukua siku inayofuata. Ivan anafungua mlango na kumuona Anna akiwa anavaa gauni la hospitali. 

Ivan kwa hasira anaanza kumkaba Pau, akimshutumu kwa kula njama.Hatimaye anasimama, akitangaza kwamba hajali tena ikiwa Pau anataka kwenda jela, Anna anajificha nyuma yake na kumchoma na kitu chenye ncha kali mara mbili. 

Ivan anavuja damu hadi kufa kutokana na jeraha la shingo yake. Pau analia akijaribu kujitetea kwa Anna,lakini Kimya Anna anasogea na kumchoma Pau na kitu chenye ncha kali mara kadhaa hadi kifo.Mwisho Anna anaonekana akitazama huku akitokwa na machozi na damu zikimtoka.

Acha comment hapo chini utuambie ni movie gani nyingine ungependa kuona Simulizi yake. 

Comments

Post a Comment